Habari TBC 1, Wanaowataja Mkapa na Kikwete Sakata la Mchanga wa Dhahabu Kukiona cha Moto
Rais Magufuli, amewaonya watu wote wanaowataja marais wastaafu, Benjamin Wiliam Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete, kuacha mara moja mchezo huo vinginevyo watakiona cha mtema kuni.
Magufuli ameyazungumza hayo wakati akizungumzia ujio wa Mwenyekiti wa kampuni ya Barrick Gold Cooperation, John L. Thornton na muafaka walioufikia kuhusu sakata la madini, hususan ishu ya kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia inayotajwa kuiingizia serikali hasara ya matrilioni ya fedha.
“Tume ilisomwa, summary yote, ilipowomwa na Profesa Mruma na hata Profesa Ossoro, majina ya Kikwete na Mkapa hayakutajwa sasa kuna magazeti yameanza kupotosha taarifa na kushupalia ishu ya Mkapa na Kikwete, sasa nawaonya, tutachukua hatua kali kwa wote wanaofanya hivyo,” alisema Mheshimiwa Rais.
#Global TV Online, kwa kushirikiana na TBC 1, wanakuletea taarifa ya habari iliyosheheni matukio mbalimbali nchi nzima.
Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1
Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…
http://www.youtube.com/c/uwazi1
http://www.youtube.com/c/uwazi1
http://www.youtube.com/c/uwazi1
WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/
FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublishers/
TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari
INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpublishers/